Uchambuzi wa 1 Samweli 24 — Pango la Engedi, Upindo wa Vazi, na Dhamiri Inayotetemeka: Rehema Inapokataa Kisasi
- Pr Enos Mwakalindile
- Dec 24, 2025
- 1 min read
Updated: Jan 6
Baada ya kunusurika kwenye "Mwamba wa Kunusurika" kule Maoni, Sauli anarudi tena kumwinda Daudi akiwa na askari teule 3,000. Katika mazingira ya miamba ya mbuzi wa mwitu kule Engedi, pambano la kifo linageuka kuwa pambano la dhamiri. Hapa, mfalme aliyewindwa anajikuta ameshika uhai wa mwindaji wake mkononi mwake ndani ya giza la pango. Sura hii inatufundisha kuwa ushindi wa kweli haupatikani kwa kumwaga damu ya adui, bali kwa kuishinda hamu ya kisasi na kuiacha hukumu mkononi mwa Mfalme wa Wafalme.





Comments