top of page



WALAWI 25 – SABATO NA MWAKA WA JUBILEI: UHURU NA UPYAISHO KATIKA KRISTO
Sabato na Mwaka wa Jubilei si historia ya kale tu; ni mwaliko wa Mungu wa kuishi katika uhuru na pumziko la kweli linalopatikana katika Kristo, tukitoa msamaha, haki na upyaisho wa maisha kwa wote.
Pr Enos Mwakalindile
2 days ago4 min read


WALAWI NA UJUMBE WAKE: NJIA YA KUKARIBIA UWEPO WA MUNGU
Walawi linafunua jinsi Mungu anavyotoa njia kwa watu wenye dhambi kuishi karibu na uwepo wake kupitia upatanisho, utakaso na wito wa maisha ya utakatifu. Kitabu hiki kinatufundisha kuwa kupitia Yesu Kristo, Kuhani Mkuu wa milele, njia ya kuingia kwenye uwepo wa Mungu sasa imefunguliwa kwa wote.
Pr Enos Mwakalindile
3 days ago4 min read


WALAWI 27 – NADHIRI NA VITU VILIVYOWEKWA WAKFU
Walawi 27 inatufundisha kuwa nadhiri na vitu vilivyowekwa wakfu si maagizo ya lazima bali matendo ya hiari yanayoonyesha moyo wa kujitoa na upendo kwa Mungu. Yesu ndiye mfano wa kujitoa kamili, na kanisa la mwanzo linaendeleza roho hii ya hiari. Maisha yetu leo yanaitwa kuwa sadaka hai, tukitimiza ahadi zetu kwa uaminifu na kumpa Mungu kilicho bora kwa shukrani na heshima.
Pr Enos Mwakalindile
3 days ago4 min read


WALAWI 26 – BARAKA NA LAANA
Walawi 26 hutufundisha kuwa chaguo la kila siku kati ya utiifu na uasi ni chaguo la kati ya uzima na mauti. Baraka kuu ni uwepo wa Mungu; hukumu kuu ni kutokuwa naye. Hata hivyo, rehema ipo kwa wote wanaorudi kwake kwa toba.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago4 min read


WALAWI 24 – TAA NA MIKATE MBELE ZA BWANA: NURU NA RIZIKI YA MUNGU KWA WATU WAKE
Taa ya daima na mkate wa uwepo vinaonyesha kwamba Mungu ndiye nuru na riziki ya watu wake. Kristo ndiye mkate wa uzima na nuru ya ulimwengu, akituita tuishi kwa heshima ya jina la Mungu na mshikamano wa kiroho kila siku.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago4 min read


WALAWI 23 – SIKUKUU ZA BWANA
Walawi 23 hufundisha jinsi sikukuu za Bwana zinavyotuongoza katika pumziko, sherehe na matumaini ya wokovu kwa Kristo, na kutukipangilia maisha yetu kwa nyakati za Mungu.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago4 min read


WALAWI 22 – UTAKATIFU WA SADAKA NA MEZA YA BWANA
Sadaka za Walawi na Meza ya Bwana zote zinatufundisha jambo moja: Mungu anataka sadaka safi, mioyo safi, na kushiriki naye katika ushirika wa kweli.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago3 min read


WALAWI 19 – UTAKATIFU KATIKA KILA SIKU
Walawi 19 unafundisha kuwa utakatifu wa Mungu unagusa maisha yote – familia, biashara, mahusiano na hata maamuzi ya kila siku. Wito wa "Mpende jirani yako kama nafsi yako" unaleta taswira ya jamii yenye upendo, haki na usawa, inayoshuhudia kuwa Mungu ndiye Bwana wa maisha yetu yote.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago4 min read


WALAWI 21 - UTAKATIFU WA MAKUHANI NA HUDUMA YA MADHABAHU
Walawi 21 inafundisha kuwa makuhani waliitwa kuishi kwa usafi wa kipekee kwa sababu walihudumu mbele za Mungu. Leo, wito huo wa utakatifu unapanuliwa kwa kila muumini, akihimizwa kuishi maisha yenye heshima na ushuhuda wa kiroho.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago3 min read


WALAWI 20 – HUKUMU YA DHAMBI NA ULINZI WA UTAKATIFU
Walawi 20 inatoa hukumu kali kwa dhambi ili kulinda maisha, familia, na heshima ya taifa la agano, na inatualika kuishi katika utakatifu wa Kristo leo.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago4 min read


WALAWI 18 – KUISHI USAFI WA MOYONI KATIKA JAMII ILIYOPOTOKA
Walawi 18 ni mwongozo wa utakatifu unaoonesha jinsi ya kuishi kwa uaminifu mbele za Mungu katikati ya jamii iliyopotoka. Ni wito wa kulinda moyo safi, mahusiano safi, na ushuhuda safi kwa dunia.
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago3 min read


WALAWI 17: KUELEWA MAANA YA “UHAI UMO KATIKA DAMU”
Uhai wetu unapatikana katika damu yetu, kiini halisi cha nafsi yetu. Basi, tunafikiria nini ikiwa kila tendo letu la kila siku linaweza kuwa dhabihu yenye thamani, yenye kuheshimu kiini hiki kitakatifu?
Pr Enos Mwakalindile
4 days ago4 min read


WALAWI 16 – SIKU YA UPATANISHO
Siku ya Upatanisho ni kilele cha Walawi: siku ya utakaso wa hekalu, makuhani, na watu wote. Leo inatutazama sisi kupitia Kristo, ambaye ameingia patakatifu pa mbinguni na kufungua njia ya pumziko na usafi wa milele kwa kila aaminiye.
Pr Enos Mwakalindile
5 days ago6 min read


WALAWI 15 – MWILI, MAJI NA USAFI WA MOYO
Walawi 15 inatufundisha kwamba usafi wa nje ni ishara ya moyo safi na maisha mapya katika Kristo Yesu, hekalu la Roho Mtakatifu.
Pr Enos Mwakalindile
5 days ago4 min read


WALAWI 14 – UTAKASO NA UREJESHO WA DHATI
Walawi 14 ni sura ya neema na urejesho, ikifundisha kuwa Mungu hashughulikii tu ugonjwa bali anarejesha mtu, nyumba na jamii kwa pamoja. Kristo ndiye utimilifu wa utakaso huu, akitupatia usafi wa moyo na uumbaji mpya wa maisha yetu yote.
Pr Enos Mwakalindile
7 days ago4 min read


WALAWI 13 - UCHUNGUZI WA NGOZI NA UCHAFU WA MOYO
Walawi 13 hufunua kwamba alama za nje mara nyingi huonyesha hali ya ndani ya moyo. Kristo anatupa utakaso na tumaini la maisha mapya.
Pr Enos Mwakalindile
Jul 254 min read


WALAWI 10– DHAMBI ISIYOSAMEHEKA: KUDHARAU UTAKATIFU WA MUNGU
Walawi 10 ni sura ya huzuni na hofu takatifu. Inatuonya kwamba si kila ibaada inapokelewa na Mungu. Moto wa kigeni ni ibaada isiyoamriwa na Bwana—na matokeo yake ni mauti. Kristo ndiye moto halisi wa madhabahu.
Pr Enos Mwakalindile
Jul 256 min read


WALAWI 11 – USAFI WA MWILI, UTAMBUZI WA ROHO
Sheria za vyakula za Walawi 11 ni mwaliko wa hekima na utakatifu: kuishi maisha yaliyotengwa kwa Mungu na kuheshimu uhai, sasa yakitimilizwa katika usafi wa moyo kupitia Kristo.
Pr Enos Mwakalindile
Jul 245 min read


WALAWI 12 - KUZALIWA NA KUTENGWA: UZAZI NA UTAKATIFU
Uzazi si najisi bali ni mwaliko wa utakaso. Katika Kristo, damu ya uzazi inapata maana mpya—si ya kutenga, bali ya kuunganisha maisha mapya na neema ya Mungu.
Pr Enos Mwakalindile
Jul 184 min read


WALAWI 9 - SADAKA YA DHAMBI
Katika Walawi 9, tunaona sadaka ya dhambi ikifungua mlango wa ibaada ya kweli. Hata kuhani mkuu lazima aanze kwa toba. Hii ni picha ya rehema ya Kristo: njia ya kurudi daima ipo wazi.
Pr Enos Mwakalindile
Jul 174 min read
bottom of page