Uchambuzi wa 2 Samweli 13 — Maandazi Gizani, Mlango Uliopigwa Komeo, na Karamu Iliyogeuka Kuwa Damu: Upanga Unapoingia Nyumbani
- Pr Enos Mwakalindile
- Jan 10
- 1 min read
Sura nyingine zinasikika kama radi nje ya mji. Hii hapa ni radi ndani ya familia. Mwana anaugua kwa kutamani. Dada anakuwa mlo uliandaliwa kwa ajili ya uongo. Mlango unafungwa kwa komeo. Binti mfalme anatoka nje akiwa amejipaka majivu. Miaka miwili inapita kama sumu ya kimyakimya. Kondoo wananyolewa. Divai inamiminwa. Na nyumba ya mfalme inajifunza kile Nathani alichomaanisha: “upanga hautaondoka nyumbani mwako.” (2 Samweli 12:10)





Comments